BurudaniHabari

Chameleon kuzindua albam ya tano

Chameleon Ikiwa ni album yake ya tano tangu aingie kwenye soko la muziki Joseph Mayanya a.k.a Jose Chameleon wa Uganda wiki ijayo anatarajia kuzindua albam yake ya tano inayokwenda kwa jina la “Shida Za Dunia”.

 

Chameleon

 

Na Daniel Nyalusi

Ikiwa ni album yake ya tano tangu aingie kwenye soko la muziki Joseph Mayanya a.k.a Jose Chameleon wa Uganda wiki ijayo anatarajia kuzindua albam yake ya tano inayokwenda kwa jina la “Shida Za Dunia”.

Albam hiyo itakuwa na nyimbo kumi na kati ya hizo kutakuwa na Classic Jazz mbili na pia amewashirikisha watanzania watatu Lady Jaydee kwenye wimbo ‘Kiboko yao’, Bwana Misosi katika ‘Walisema’ na katika wimbo ‘Mama Rhoda’ anasema amemshirikisha Bushoke ingawa Bushoke anadai Chameleon amemfanyia uhuni kwa kubadilisha uhalali wa kushirikishwa na yeye kuwa ndio mmiliki wa nyimbo hiyo.

Pia katika albam hiyo kuna nyimbo ya ‘Bomboclact’ ambayo ameiba beat ya ‘Nikusaidiaje’ ya Prof. Jay, wimbo wa ‘Shida za Dunia’ unaobeba jina la albam na wimbo wa ‘Maoko na Maoko’ ambayo ametumia lugha ya Kishona ya Wazimbabwe.

Albam hiyo inayotarajiwa kuzinduliwa kwa awamu mbili itaanza kuzinduliwa tarehe 16 katika ukumbi wa Africana Hotel na siku itakayofuata itazinduliwa Gaba Beach .

{mos_sb_discuss:6}

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents