Habari

Changamoto mpya zaanza kujitokeza kwenye vituo vya mabasi yaendayo kasi

Baada ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuanza kulipia nauli tangu jana [Jumatatu] kwenye mabasi yaendayo kasi changamoto nyingi zimeanza kujitokeza kwenye vituo hivyo.

IMG_5542

Abiria wamelalamikia serikali kutokana na usumbufu wanaoupata kwenye vituo hivyo ikiwemo upatikanaji wa triketi za kupandia gari. Kwenye vituo kadhaa vya mabasi hayo vimeonekana abiria wakiwa wameweka foleni kwa ajili ya kukata tiketi huku wengine wakiwa wameweka foleni ya kusubiria kurudishiwa chenji.

Mmoja wa maafisa wa mradi huo [UDART], Deusi amesema changamoto hizo wameziona zimejitokeza kwenye baadhi ya vituo ikiwemo kituo cha Ubungo na Mbezi.

“Mfumo huu wa tiketi uliwekwa kwa dharura tu, mfumo unaotakiwa kutumika ni wakadi kama mtu anatumia kadi ni rahisi kwake hataweza kupata usumbufu kama huu. Tulitegemea tiketi zitakuwa kwa wale wateja wa dharura tu lakini badala yake watu wengi ndio wanaotumia mfumo huu. Changamoto nyingine kwenye vituo vyetu ni chenji imekuwa na shida sana ndio maana foleni imezidi kuwa kubwa,” alisema.

Hata hivyo viongozi wa mradi huo wamesema kuwa wameiona changamoto hiyo na watajitahidi kuitatua ndani ya muda mfupi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents