Changamoto za Mazingira

 

Mradi wa Hifadhi ya Mazingira ya ziwa Tanganiyika unakabiliana na chngamoto mbali mbali zitokanao na mabadiliko ya Tabia Nchi ambayo hupelekea Ogezeko la jua, mvua ambazo pia huleta athari kubwa sana katika mazingira hayo.

Hayo yameelezwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Rais anaeshughulikia Mazaingira Mh Dkt Batilda Burian alipokuwa akifungua mkutano wa wadau uliokuwa ukizungumzia namna ya kukabialana na changamoto hizo, uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Dkt Batilda ameeleza kuwa, mbali na suala la mabadiliko ya tabia nchi mazingira ya mradi wa ziwa Tanganyika yanakabiliwa pia na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja na shughuli za kibinadamu ambazo husababisha upungufu wa kina cha maji katika ziwa na aliongeza kuwa maji machafu yanayoingia katika ziwa si salama kwa viumbe hai waishio ziwani pamoja na binadamu.

Mh. Batilda aliongeza kwa kusema kuwa, Ongezeko la watu katika miji inayozunguka ziwa Tanganyika pia ni tishio kwa mazingira hayo kwani  hufanya huvuvi haramu na kilimo holela “hivyo basi jitihada mbali mbali zinahitajika kufanyika hili kukabiliana na changamoto hizi na ndo mana wadau  hawa wanakutana hapa leo Alisisitza.”

Mkutano huo unaofadhiliwa na Mfuko wa Mazingira wa Dunia (GEF) shirika la maendeleo la umoja wa mataifa (UNDP) unahusisha wadau mbali mbali kutoka nchi zinazozunguka ziwa Tanganyika, Wizara mbali mbali, UDSM, NGOs na Taasisi za Serikali.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents