Habari

Chanjo ya homa ya Ini kupatikana kwa wananchi

Waziri wa afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa chanjo ya homa ya Ini inatarajiwa kupatikana kwa wananchi wote bila kujali kigezo cha umri, uwezo wa kifedha kwa wananchi wenye hatari au ugonjwa wa ini kwa bei nafuu mpaka kufikia mwaka 2020.

Waziri Ummy amezungumza hayo, katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusu maadhimisho ya ugonjwa wa homa ya ini duniani.

“Katika kuadhimisha siku ya ugonjwa wa homa ya ini duniani tumedhamiria kuhakikisha chanjo ya ugonjwa huu inapatikana kwa watu wote nchini ambao wana hatari ya kupata maambukizi ya homa ya ini au tayari wamepata ugonjwa huo kwa bei nafuu kwa mswaka wa bajeti 2018/2019,” alisema Waziri Ummy.

Hata hivyo alisema kuwa chanjo ya homa ya Ini kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano inapatikana hapa nchini kwenye vituo vya huduma ya afya vya serikali na watu binafsi.

Aidha Ummy alisema kuwa ili kujilinda na maambukizi ya ugonjwa wa homa ya ini mpango wa damu salama unatakiwa kuhakikisha wanapima damu zote za wachangiaji kabla ya kuwawekea wagonjwa wanaohitaji huduma ya damu.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents