Channel O kutoa milioni 12

Shindano la kumsaka mnenguaji bora wa muziki wa dansi linalotarajiwa kufanyika hapa nchini mwishoni mwa mwezi huu likiwa limeandaliwa na kituo maarufu Channel O, ambapo mshindi kujibebea kitita cha shilingi milioni 12 pasi na kipingamizi

Shindano la kumsaka mnenguaji bora wa muziki wa dansi linalotarajiwa kufanyika hapa nchini mwishoni mwa mwezi huu likiwa limeandaliwa na kituo maarufu Channel O, ambapo mshindi kujibebea kitita cha shilingi milioni 12 pasi na kipingamizi



Akizungumza kwa njia ya simu mmoja wa waratibu wa shindano hili bwana Khadoni alidai kuwa shindano hili litashirikisha nchi mbali mbali za afrika ikiwemo Nigeria, Ghana, Kenya, Namibia pamoja na Tanzania na kila nchi itatoa washindi wawili watakaokwenda Afrika Kusini kwa ajili ya fainali.



Shindano hilo ambalo limeandaliwa na kituo cha Televisheni cha Channel O cha Afrika Kusini, linatarajiwa kufikia tamati mwishoni mwa Mei, mwaka huu.
“Washiriki ambao watashinda kwenda kushiriki katika Fainali, wanatarajia kukaa nchini humo kwa kipindi cha mwezi mmoja wakifanya maandalizi ya fainali hizo za kumsaka mnenguaji bora barani Afrika”-Khadomi.



Khadoni alisema mbali ya mshindi kuzawadiwa kitita hicho cha sh milioni 12, pia atapata nafasi ya kujifunza mambo mengi yanayohusiana na sanaa hiyo ya unengeaji wa aina mbali mbali za muziki.



Mpaka sasa ni washiriki kibao ambao wameshajitokeza kwenye ukumbi maarufu jijini wa Club Maisha kwa ajili ya kuchuana, baadhi yao ni pamoja na Rubins, Khalid, Mohammed, Freddy, Maria, Suzan, Peter na wengineo wengi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents