Burudani

Chanzo cha kifo cha muigizaji John Heard wa ‘Home Alone’ chabainika

Chanzo cha kifo cha John Heard muigizaji wa‘Home Alone’ aliyefariki Julai 21 mwaka huu mjini California kimebainika kuwa ni shinikizo la moyo.

John alifanyiwa upasuaji katika kituo cha afya cha Stanford Medical Cente, na kisha kuelekea hoteli ya Palo Alto iliopo katika mji huo,baada ya siku mbili ndipo umauti ukamkuta.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na hospitali ya Santa Clara County Medical, baada ya uchunguzi umebaini kuwa kifo chake kimetokana na shinikizo la moyo.

Marehemu amekutwa na umauti akiwa na miaka 72, na ameacha mke Margot Kidder na mtoto wake mmoja aitwaye John Matthew “Jack”.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents