Burudani

Chanzo: Drake na Rihanna wadaiwa kupigana chini tena.. kisa Chris Brown

Story ya Rihanna, Drake, Chris na Karrueche Tran imekuwa kama ile hadithi ya Pwagu na Pwaguzi.

Rihanna+Drake+2011+NBA+Star+Game+Performances+vX7jhakwkZQl
Ni juzi tu hapa vyombo vya habari mtandaoni viliandika kuwa Drake na Rihanna ni wapenzi na wameamua kuuchukulia uhusiano huo serious zaidi. Na sasa vyanzo vinadai kuwa wawili hao wamezinguana tena – kisa Chris Brown. Chanzo cha uhakika kimeuambia mtandao wa Urban Islandz kuwa Rihanna amekuwa akiwasiliana na Chris Brown ambaye hata hivyo kwa sasa yupo jela.

Chris+Brown+New+York+Knicks+v+Los+Angeles+SGpYZxN7G7il

“Robyn bado anampenda sana Chris na Drake alishtukia kuwa amekuwa akiwasiliana naye,” chanzo kilisema. “Siku moja alimsikia akiongea na Chris na kumfokea lakini Riri alikanusha kuwa na uhusiano na Chris. Kisha aligundua kuwa Rihanna na Chris wamekuwa wakitumia jumbe za mapenzi na kumfanya akasirike kiasi cha kuamua kuvunja tena.”

karrueche-tran-chris-brown-insta-new-year__oPt

Chanzo hicho kimedai pia kuwa Karrueche Tran alimpiga chini Brown alipogundua kuwa alikuwa akimtumia sms za mapenzi Rihanna.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents