BurudaniHabari

Chapakazi ubaoni na ‘Okoa’

Adili a.k.a HisabatiMkanda mpya wa video za wasanii wa kizazi kipya ambazo hazijawahi kuonekana katika kituo chochote cha luninga unaoandaliwa na kampuni ya utengenezaji wa video ya Chapakazi

Adili a.k.a HisabatiMkanda mpya wa video za wasanii wa kizazi kipya ambazo hazijawahi kuonekana katika kituo chochote cha luninga unaoandaliwa na kampuni ya utengenezaji wa video ya Chapakazi unatarajiwa kukamilika hivi karibuni na kutupwa sokoni.

 

Akizungumza na Bongo5 mmiliki wa kampuni hiyo ambaye pia ni msanii wa Hip hop hapa nchini Adili a.k.a Hisabati alisema “hivi sasa naandaa mkanda wa video utakaojulikana kwa jina la okoa ambao utakuwa ukionesha na kuelezea kwa kifupi kuhusu wasanii wa Hip hop nchini Tanzania ”

 

Unatarajiwa kuwa katika mfumo wa DVD ambayo itawahusisha wasanii kibao na video zao ambazo hazitachezwa kwenye kituo chochote cha luninga isipokuwa katika mkanda huo utakaopatikana katika soko la muziki hapa nchini.

 

Wasanii ambao wanatarajiwa kuonekana pamoja na kazi zao ni pamoja na Fid Q, Joh Makini, Mapacha, Mansu-li, Salu-Te, Mwana Fa, Sugu, Big 4 De Gz na wengine nyomi wanaofanya Hip Hop.

 

Source: Bongo5

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents