Michezo

Mkwasa apewa mkataba rasmi kuinoa Taifa Stars

TFF imefikia makubaliano na kocha Charles Boniface Mkwasa ya kumpa mkataba rasmi baada ya kuridhika na utendaji wake katika kukinoa kikosi cha timu ya Taifa Stars.

Mkwasa-Master

Mkwasa amepata mkataba wa kuifundisha timu hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu kuanzia Oktoba Mosi mwaka huu na kumalizika Machi 31, 2017.

Baada ya kusaini mkataba huo, Mkwasa sasa atapatiwa huduma na marupurupu yote aliyokuwa akipewa kocha aliyeondoka.

Mkwasa ameeleza kufurahishwa na makubaliano hayo na ameahidi kufanya kila jitihada kuhakikisha kiwango cha timu ya Taifa kinapanda. Aidha Kocha ametoa wito kwa wadau wa mpira kumpa ushirikiano katika majukumu yake mapya.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents