Habari

Chaz Baba aka Mr President


Nyota wa muziki wa dansi ‘Chaz Baba’ ameendelea kungara katika bendi ya Mashujaa baada ya juzi kuchaguliwa kuwa raisi wa bendi hiyo.

Mwanamuziki huyo alichaguliwa katika uchaguzi wa wazi na haki uliofanywa na wanamuziki wa bendi hiyo,ambapo Chaz aliibuka kidedea.

Chaz alimshinda mpizani wake kwa kura 19 kati ya kura ishirini zilizopigwa na wanamuziki wote, wakati wakiongozwa na msimamizi ambaye pia ni mnenguaji Sweety Baby.

Katika kinyanyiro hicho alikuwa akichuana na wanamuziki wenzake sita akiwemo, Jumanne Nyamwela, Milinda Nyeusi, Sauti ya Radi, Amos ‘Mpiga Solo’ na wengine.

Hongera Mr. President Chaz Baba!!

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents