Burudani

Chaz Baba ameguka Twanga Pepeta

twanga_waimbaji

Bendi ya Twanga Pepeta imejikuta ikianza mwaka 2012 vibaya baada ya mwanamuziki wake tegemezi katika upande wa waimbaji Chazi Baba kutangaza kujitoa katika bendi hiyo baada ya mkabata wake kuisha kwa muda mrefu na kupiga akapela.

Chazi Baba amesema kwamba tangu mwaka 2006 mwezi wa pili, ndiyo mwisho wa kusaini mkataba wake hivyo akawa anaitumikia bendi hiyo kama vile mtu wa kawaida ambaye anajitolea. Amesema kwa sasa ameamua kutafuta Meneja kwaajili ya kusimamia kazi zake na mikataba yake yote yatakayo husiana na kazi zake.

Pia amesema sasa hivi yupo huru kwenda Bendi yoyote ambayo inamtaka,  ila cha msingi na kufuata masharti ambayo atakubaliana na meneja wake huyo.

Amesema wasanii wengi wamekuwa wakifanya kazi bila ya mafanikio kwakuwa wamekuwa hawajui haki zao za msingi, na hatmaye kujikuta mwisho wa siku wakiitumikia bendi na wao kuambulia umaskini. Pia ameongeza kwa kusema meneja wake anaitwa Benard Msekwa, na ndiyee takuwa msimamizi wa kazi zake zote kwakuwa amesomea sheria.

kwa sasa anatarajia kwenda Dudai kwaajili ya mapumziko ya wiki tatu, na baada ya hapo atarudi kwaajili ya kuendelea na kazi hiyo ya kimuziki kama atakuwa tayari ameshapata bendi. hata hivyo amekiri kwamba yupo radhi kubakia Twanga Pepeta kwa kuwa bado anaipenda

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents