Burudani

Chege amuombea Recho collabo na Wahu

chege page

Chege Chigunda ameamua kumwombea collabo msanii wa ‘Nashukuru Umerudi’ Recho wa THT kwa Wahu Kagwi wa nchini Kenya.

Chege ambaye amewahi kumshirikisha Wahu kwenye hit yake ‘Mkono Mmoja’ na yeye (Wahu) kumshirikisha kwenye remix ya ngoma yake Running Low, ametumia Twitter kuwakilisha ombi la Recho.

“Niko poa sana wangu!huku bongo kuna artisti anaitwa recho hivi unamfahamu? Anafanya poa sana huku bongo anataka kufanya colabo,” ametweet Chege.

Chege twwt

Hata hivyo baada ya hapo mazungumzo ya mastaa hao yameendelea pembeni na bila shaka muda si mrefu tutasikia ngoma ya Recho aliyomshirikisha Wahu. Ni ngumu kushindwa kushawishiwa na sauti tamu ya Recho.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents