Burudani

Chege kuachia albamu yake wiki hii

Msanii wa Bongo Flava, Chege amethibitisha ujio wa albamu yake yenye ngoma zaidi ya kumi itakayotoka ifikapo Ijumaa hii.

Chege anayetamba na ngoma yake mpya ya ‘Run Town’ amekieleza kipindi cha Daladala Beat ya Magic Fm, kuwa ifikapo Ijumaa atatoa rasmi albamu yake.

“Ijumaa na dondosha albamu ya Run Town, hii ni albamu yangu ya nne katika muziki, kwa sasa bado tupo kwenye kikao cha mwisho cha kujadili albamu hii ipatikane sehumu gani,” amesema msanii huyo.

Katika mahojiano aliyowahi kufanya hivi karibuni Chege aliwahi kusema kuwa moja ya msanii atakaye sikika katika albamu yake ni rapper Chid Benz pia kutakuwa na kolabo mbalimbali na wasanii wa Nigeria, Afrika Kusini na nchi zingine.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents