Burudani

Chege, Young Killer, Bob Junior wawasihi wananchi kujiandikisha na kupiga kura

Young Killer, Chege na Bob Junior wamewataka watanzania kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ili wapate haki yao ya msingi ya kupiga kura na kuwachagua viongozi wanaowataka.

Young Killer, Chege na Bob Junior

Wakizungumza na Bongo5 leo kwa nyakati tofauti wasanii hao wasema kila mtanzania anapaswa kujiandikia ili asikose haki yake ya kuchagua viongozi.

Young Killer

Tujitokeze tukajiandikeshe kwa sababu kiongozi bora wa kwako unamfahamu wewe, usije ukashindwa kujitokeza halafu ukashindwa kupiga kura na kukosa haki yako ya msingi ya kuchagua kiongozi wako, halafu ukaanza kulaumu watu ‘ooh kiongozi hafai’ wakati hukutumia haki yako ya kuchagua kiongozi sahihi. Kwahiyo ni muda mzuri na muda muafaka na ni nafasi yako kila mtanzania kujiandikisha na kupata kazi ya kuchagua viongozi bora. Kwahiyo ni vyema watu tukajitokeza kwa wingi na tukajiandikisha.

Bob Junior

Mimi nachotaka ni amani zaidi. Tumekuwa tukiona matukio mbalimbali katika nchi zetu za jirani katika uchaguzi. Tuweke pembeni tofauti zetu za kisiasa na tuamue kuchagua viongozi wazuri. Lakini haya yote tuwe tuyafanya kama watanzania tutashindwa kujiandikisha katika daftari la kudumu ya wapiga kura. Kwahiyo kila mtanzania ajiandikishe ili apate haki ya kupiga kura.

Chege

Huu ni wakati wetu sasa watanzania wa kujiandikisha na kupiga kura. Usipofanya hivyo utakosa haki yako yako ya kupiga kura. Kwahiyo tuache kuongea na kulaumiana kuhusu viongozi wetu. Twendeni tukajiandikishe kwa pamoja ili tuchague viongozi wetu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents