Shinda na SIM Account

Cheka adai hakupigwa India, aeleza alichofanyiwa na mwamuzi

Bondia Mtanzania Francis Cheka ambaye mwishoni mwa wiki alipoteza pambano lake nchini India alilopigana na raia wa nchi hiyo Vijender Singh, ameibuka na kusema kuwa mpinzani wake huyo hakumpiga, ila alibebwa na mwamuzi.

Akiongea katika kipindi cha 5Sports cha EATV kwa njia wa simu kutoka nchini India, Cheka amesema katika raundi hiyo ya tatu, alipata tatizo katika kifaa chake cha kulinda meno kwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na kikohozi, na wakati anakifanyia marekebisho, ndipo mwmuzi akatangaza mshindi, bila kumuuliza Cheka mwenyewe kama alikuwa anaendelea au la.

“Tatizo nilikuwa nakohoa, nilijiandaa vizuri kumpiga yule Vijender,” alisema Cheka.

Pia katika mtandao wake wa Instagram aliandika:

Pale ambapo matokeo yamepangwa, tunaenda kukamilisha ratiba tu, Refa unaona mouth guard imetoka na unaendelea kuchezesha… Watanzania nadhani mmeona, tusiwage wanyonge kwao na kwetu pia… Nadhani nimeliwakilisha taifa vyema, kuitangaza Morogoro, Tanzania, Kiswahili na Kimakonde pia.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW