Michezo

Cheka afunguka baada ya kudundwa ‘Sijui kilichotokea, nilijikuta tu niko chini’

Bondia Francis Cheka amekubali yaishe kwa Abdallah Pazi (Dullah Mbabe)  baada ya kuchapwa kwa Knock Out raundi ya sita ya pambano lililokuwa la raundi 12 la kuwania ubingwa wa mabara wa wa WBF kwenye uzani wa super middle.

“Sijui kilichotokea,  Nilijikuta tu niko chini raundi ya sita na sikuendelea tena na pambano, ” Cheka aliliambia gazeti la Mwanaspoti.

Katika pambano hilo lililopigwa kwenye ukumbi wa PTA, Sabasaba mashabiki wa Cheka waliduwazwa na kipigo hicho hevi.

“Sina namna zaidi ya kukubaliana na matokeo, Nimepigwa kihalali, sijui nilipatwa na nini kwani sikuwa natembea ulingoni,  Muda mwingi nilicheza kwenye kamba wakati si kawaida Yangu,.

Cheka alidai kipigo chake hakijasababishwa na umri au kiwango chake kushuka isipokuwa mpinzani wake alimuotea tu na kushinda.

“Hadi sasa sijui nimepotezaje pambano hilo, lakini pamoja na kupoteza siwezi kustaafu ngumi kwa sasa, ” alisema.

Hata hivyo Dullah Mbabe Ametamba kwamba kipigo hicho kwa Cheka si cha kubahatisha alijiandaa kumnyamazisha bondia huyo bingwa wa zamani wa dunia wa WBF.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents