Tupo Nawe

Chelsea kumruhusu N’Golo Kante kubaki nyumbani mpaka pale atakapojisikia kurudi klabuni

Chelsea imejiandaa kumruhusu nyota wake N’Golo Kante kuukosa msimu mzima uliosalia wa 2019-20 kwa kubaki nyumbani kama atakuwa anahofia virusi vya Corona.

N'Golo Kante (pictured, second left) attended training on Tuesday but is now staying at home

Hapo siku ya Alhamisi kiungo huyo alikuwepo katika viwanja vya mazoezi baada ya kufanyiwa vipimo lakini kwa sasa mchezaji huyo ameamua kubaki nyumbani tangu alivyoonekana hiyo juzi kwa kuhofia afya yake juu ya janga hili.

Chelsea are reportedly prepared to let the midfielder miss the rest of the 2019-2020 season

Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 29, siku chache zilizopita alipita katika kipindi kigumu za kiafya kwa kuondokewa na kaka yake ambaye amekufa kwa shinikizo la moyo, hivyo kwa mujibu wa The Sun, Chelsea itamuacha mchezaji huyo mpaka pale atakapo amua mwenyewe kiurudi klabuni.

The Frenchman has had previous health issues and is nervous about resuming football

Kante amekuwa mchezaji mwenye umuhimu mkubwa ndani ya the Blues akiwa amecheza jumla ya michezo 18 na kutupia magoli matatu kunako Premier League msimu huu.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW