Michezo

Chelsea kumtimua Conte na huyu ndiye kocha atakayerithi mikoba yake

Klabu ya Chelsea ipo mbioni kumtimua kocha wake, Antonio Conte hii ni baada ya kuonekana kocha huyo mpaka sasa kushindwa kuongeza mkataba na klabu hiyo.

Tokeo la picha la antonio conte
Antonio Conte

Inasemekana kuwa Antonio Conte amekuwa na majanga mengi tangu Chelsea ilipotwaa ubingwa msimu uliopita na hayuko katika mahusiano mazuri na wachezaji klabuni hapo.

Conte amekuwa na madai mengi ndani ya klabu ya Chelsea kuhusu masuala ya usajili na mambo mengine mengi ikiwemo masuala ya Akademi ya soka ya Chelsea.

Gazeti la The Sun la nchini England limeandika kuwa Conte amekuwa chanzo cha Chelsea kuzinguana na Diego Costa na matatizo haya yote yanamuweka Conte njia panda kuendelea kuinoa klabu hiyo.

Kwa mujibu wa gazeti la Bild la nchini Ujerumani limeripoti kuwa tayari viongozi wa klabu ya Chelsea wameshanya maongezi na kocha wa zamani wa klabu ya Borussia Dortmund, Thomas Tuchel kurithi mikoba ya Muitaliano, Antonio Conte.

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents