Michezo

Chelsea waichomolea Barcelona kwa Willian

Klabu ya Chelsea imekataa ofa ya pauni milioni 50 kutoka kwa Barcelona kunasa saini ya kiungo wa timu hiyo Willian.

Mchezaji huyo raia wa Brazil amehusishwa kutimka Stamford Bridge kwa zaidi ya miezi kadhaa sasa.

Willian mwenye umri wa miaka 29, amekuwa pia akiwindwa na klabu ya Manchester United wakati huo huo Barcelona ikihitaji huduma ya kiungo huyo.

Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari Barca imekuwa katika ushindani mkubwa na Mashetani wekundu juu ya nyota huyo wa Chelsea.

Barca ambayo imechomolewa kiasi cha pauni milioni 50 kutoka kwa The Blues inahaha kutafuta wachezaji ili kuimarisha kikosi chake kwaajili ya msimu ujao wa ligi na michuano mingine mikubwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents