Michezo

Chelsea yaichakaza Tottenham kombe la FA

Chelsea iliizaba Tottenham mabao 4-2 na kujikatia tiketi ya fainali ya kombe la FA dhidi ya mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Arsenal dhidi ya Manchester City.

Eden Hazard akishangilia bao

William aliiweka mbele Chelsea kunako dakika ya sita kwa kupiga mkwaju wa adhabu kabla ya kuongeza la pili kwa njia ya penalti kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.

Harry Kane alikuwa amesawazisha kutoka kwa krosi iliopigwa na Christian Ericksen kwa Suprs ambao walisawazisha tena kupitia bao la Delle Ali.

Mchezaji wa ziada Eden Hazard aliiweka Chelsea mbele kwa mara ya tatu kabla ya Matic kufunga bao la nne na kuiweka kifua mbele Chelsea.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents