Michezo

Chelsea yakubali kumuachia Juan Mata kwenda Manchester United

Klabu ya Chelsea imekubali kumuachia Juan Mata kwenda Manchester United na atasaini mkataba wa miaka 4 na nusu kuichezea timu hiyo.

juan-mata-455472

Ripoti zinasema United imetumia takriban kitita cha pauni milioni 37 kumsajili kiungo huyo wa Chelsea,huku kocha wa The Blues José Mourinho akiwa mbioni kumsajili kiongo wa Real Sociedad’s Antoine Griezmann.

Mata mwenye umri wa miaka 25, anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu baadaye hii leo, kabla ya kukamilisha usajili huo. Mchezaji huyo kutoka Hispania anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka minne na nusu na klabu hiyo iliyo na makao yake katika uwanja wa Old Trafford.

Mata ambaye aliichezea Chelsea, mechi 32, aliwaaga wachezaji wenzake na wakufunzi wa Chelsea katika uwanja wao wa mazoezi wa Cobham siku ya Jumatano. Hata hivyo kocha wa Manchester United David Moyes baada jana kuendelea ya kupokea kipogo kutoka kwa Sunderland katika ligi ya Capital one,alishindwa kuongelea uhamisho wa Juan Mata ambaye ni kiungo mshambuliaji.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents