Chelsea yasemekana kumtema Drogba

Chelsea yasemekana kumtema Drogba
Baada ya Didier Drogba kuomba msamaha kuna habari zimeibuka kuwa Klabu ya Chelsea iko mbioni kumtema
mchezaji huyu kwa kumuuza kwa Klabu yeyote
itakayotoa donge nono

Hii inatokana na kitendo cha mchezaji huyo hivi
karibuni kutoa maneno machafu mbele ya hadhara (dunia) kupitia Luninga
kwenye mtanange wa Ligi ya Mabingwa (Champions League) dhidi ya timu ya
Barcelona katika kuwania nafasi ya kucheza Fainali na Mabingwa watetezi
Manchester United.

Drogba ambaye kama washabiki na wachezaji wengine
alikerwa na kitendo cha refa kukataa Penalti nne kwa timu yake
ya Chelsea na uamuzi kwenye mechi hiyo ambao umesemekana ulipelekea timu ya Chelsea kupoteza mchezo huo.

Pamoja na kuomba msamaha bado kikao cha Uongozi
kitaamua hatua zaidi ya kuchukua kama Klabu kwa Drogba ambaye
ameonyesha utovu wa nidhamu na dharau kubwa, “…"Nilipandwa na mori na
kujikuta ninatamka maneno yasiyostahili. Ninaomba msamaha," alisema
Drogba. "Ninakiri kwamba matamshi yangu hayakufaa na hayakutoa mfano
mzuri kwa wale waliokuwa wakitizama televisheni, hasa watoto." alisema
Drogba kwenye maelezo yake kwa uongozi na maelezo kama hayo
yaliyokaririwa kwenye mtandao wa Klabu hiyo.

Mchezaji huyo analipwa mshahara wa Paund 91,000 kwa wiki kwa sasa na kumfanya kuwa miongoni mwa wachezaji aghali pia.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents