Chelsea yaweka rekodi nyingine kubwa EPL baada ya ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Huddersfield Town

Klabu ya Chelsea imefungua Ligi Kuu England (EPL) kwa kishindo baada ya kuichapa goli 3-0 klabu ya Huddersfield Town ugenini. Ushindi ambao umewafanya Chelsea waweke rekodi usiku wa jana.

Kwa ushindi huo, Chelsea inakuwa klabu ya tatu katika historia ya EPL kufikisha alama (points) 800 kwenye michezo ya ugenini pekee.

Rekodi hiyo ya klabu zilizovuna alama nyingi zaidi ugenini kwa sasa inashikiliwa na Man United (925) ambapo klabu nyingine ni Arsenal (800) ambao leo wanashuka dimbani kuvaana na Man City.

Kabla ya mchezo wa jana Chelsea walikuwa na alama 799 ambao waliposhika wakafikisha alama (802) kwenye michezo yao yote waliyocheza ugenini. swali ni je, kwa msimu huu huenda wakapunguza gepu lilipo  kati yao na Man United?.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW