Chemical aizungumzia Movie yake na Wema Sepetu (+audio)

Msanii wa muziki Bongo, Chemical amefunguka sababu iliyopelekea kufanya movie na muigizaji Wema Sepetu.

Chemical amesema licha ya kutoa ngoma ‘Mary Mary’ aliamua kutumia title hiyo katika movie yake hiyo na kufanya na Wema ni kutokana na sababu za kibiashara.

“Alipenda stori na kuna watu wa karibu waliongea naye na yeye aliona ni biashara sio tu kuangalia ukubwa au jina la msanii, kwa hiyo tumemfuta Wema Sepetu kibiashara,” amesema Chemical.

“Mimi sio msanii wa Bongo Movie, mimi nafanya muziki, kwa hiyo ile nimefanya kama by the way,” amesisitiza.

Ameongeza kuwa hajasita kuachia movie hiyo licha ya kuwepo stori kuwa soko la Bongo Movie limeshuka kwani movie yao ‘Mary Mary’ ina story nzuri pamoja na muziki, hivyo anakutanisha mashabiki wake na wale wa Wema Sepetu.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW