Burudani

Chidi Benz ahukumiwa kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini

Hakimu wa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, leo ametoa hukumu ya kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini kwa rapper, Chidi Benz.

DSC_0995

Chidi alipandishwa kizimbani mahakamani hapo kusomewa mashtaka matatu ya kukutwa na madawa ya kulevya mwaka jana. Alikuwa nje kwa dhamana ya shilingi milioni 1 pamoja na wadhamini wawili wasiokuwa na hatia.
Faini anayotakiwa kulipa ni shilingi laki tisa.

Chidi alikutwa na madawa ya kulevya aina ya heroin yenye thamani ya shilingi 38,638, na bangi yenye thamani ya shilingi 1,720 pamoja na na vifaa ya kuvutia dawa hizo ambavyo ni kijiko na kigae.

Tukio hilo lilitokea October 25 mwaka jana katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa anaelekea jijini Mbeya kwenye show.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents