Diamond Platnumz

Chidi Benz: Mimi ni ‘the best rapper’ hata kama nimetoboa pua

Inaonekana wimbo mpya wa Ney wa Mitego aliomshirikisha Diamond umekitonesha kidonda cha Chisd Benz kilichokuwa kimekauka tayari baada ya Diamond kukumbushia kitendo cha rapper huyo kutoboa pua.

Chidi-Benz-12

Ikumbukwe kuwa Ney wa Mitego aliwahi kumdiss Chidi kwenye wimbo wake ‘Nasema Nao’ kwa kutoboa pua yake.

Baada ya jana Ney kuachia wimbo wake huo mpya ‘Muziki gani’ na Chidi kusikia mashairi ya Diamond amelazimika kuutumia mtandao wa Facebook kusema alivyojisikia na kusisitiza kuwa bado ataendelea kuwa rapper bora licha ya kufanya hivyo.

“Mimi ni Best..kutoboa pua si kitu if imekua mada..nina watu wengi wanaonisikiliza na kuniheshim na nina waheshim pia, Naweza kufanya Muziki na nimewahi kuwafurahisha wengi. Love kwa fanz woote. La Familia,” aliandika Chidi.

“Najua nina watu wangu. Wanaamini,haki ya Mungu wanaamini. Heshima haiwezi shuka kwa mimi kutoboa pua,kuna vitu heshima inabidi ikushuke.unajua! Bythwy nina watu wangu.hio ndio point.”

Hata hivyo Diamond alisema aliongea kwanza na Chidi Benz kuhusu mstari huo kabla wimbo haujatoka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents