Burudani

Chidinma azungumzia kufanya kazi na Joh Makini kwenye ‘Perfect Combo’

Miongoni mwa nyimbo zilizofanya vizuri mwaka jana nchini ni Perfect Combo ya Joh Makini akimshirikisha staa wa Nigeria, Chidinma.

Wimbo huo haukuishia tu kufanya vizuri bali pia ulitengeneza msemo maarufu uliotokana na jina lake. Chidinma alizungumza hivi karibuni na mtangazaji wa Amka na Choice FM, Divine Kweka na kumuelezea alivyojisikia kufanya kazi na Joh Makini.

“Working with Joh Makini was so much fun,” amesema.

“I remember I was in Kenya when we recorded the song and then we went to South Africa to shoot the video, he told me how well the song is doing,” ameongeza.

Kwa upande mwingine muimbaji huyo amesema ataanza kujiandaa na album yake mpya hivi karibuni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents