Burudani

Chikune wa Namibia amtaja msanii wa Bongo Fleva aliyefanya naye Kolabo

Msanii Chikune kutoka Namibia amethibitisha kufanya kolabo na msanii wa Bongo Fleva.

14272178_1190561407652503_43807192_n

Muimbaji huyo ambaye amefanikiwa kushinda tuzo ya Afrimma mwaka huu ameiambia Bongo5 kuwa tayari ameshafanya kolabo na msanii mmoja wa kike kutoka Tanzania ambaye anatarajia kupata connection za huku.

“Kwa kuanzia nimeshafanya kolabo na Kleyah. Ni msanii wa pekee sana na anaangalia zaidi biashara na naamini ana nafasi kubwa ya kwenda sambamba kwenye tasnia ya muziki iliyotawaliwa na wanaume. Lakini pia tumeweza kuunganisha elimu kwa pamoja,” amesema Chikune.

Chikune ameongeza kuwa ana mipango ya miaka mitatu mbele ya kuitangaza brand yake Afrika na kuufanya muziki wa Namibia kujulikana zaidi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents