Burudani

Childish Gambino azua utata kwenye video ya wimbo wake mpya ‘Feels like Summer’, amliza Kanye West (+video)

Baada ya kutamba na ngoma yake ya ‘This is America’, Rapper Childish Gambino ameachia video ya wimbo wake mwingine mpya wa ‘Feels like Summer’. Wimbo ambao video yake imezua gumzo kwa sasa nchini Marekani.

Kwenye video hiyo ambayo ipo kwenye mfumo wa Animation inamuonesha rapper Kanye West akikumbatiwa na mke wa Rais Mstaafu wa Marekani, Bi. Michelle Obama huku akibubujikwa na machozi.

Kikaragosi hicho kinachofanana na Kanye West pia kinaonekana kuvalia kofia iliyoandikwa ‘MAKE AMERICA GREAT AGAIN’ sawa kabisa na kofia ambayo Rais wa Marekani huwa anaivaa.

Related image
Rais wa Marekani, Donald Trump.

Watu wengi waliotoa maoni juu ya video hiyo yenye masaa 22 tangu iachiwe mtandaoni, wameonesha kufurahishwa na jinsi Kanye West alivyolia huku wakieleza kuwa ujumbe huo bila shaka utamfikia muhusika.

Mapema mwaka huu wakati akihojiwa na TMZ, rapper Kanye West alikaririwa akisema ‘watu weusi walifanywa watumwa miaka ya nyuma nchini Marekani walichagua maisha hayo‘ kauli ambayo iliibua hasira kwa jamii ya watu weusi nchini Marekani.

Kitendo cha Kanye West kutamka kauli hiyo kilipelekea watu wengi kutomuunga mkono hata kwenye manunuzi ya ngoma zake, jambo ambalo limemfanya  wiki iliyopita kuomba msamaha kwa kauli hiyo kupitia kipindi cha The  WGCI Morning Show.

Pia, Kanye West amekuwa ni rapper wa kwanza mweusi nchini Marekani kutamka wazi kuwa anaunga mkono jitihada za Rais Trump, ambaye anapingwa vikali na jamii ya watu weusi nchini humo wakidai kuwa serikali yake ni ya kibaguzi.

Kwenye video hiyo pia inamuonesha Nicki Minaj akicheza gemu na Travis Scott, ambao wawili hao siku za hivi karibuni wameripotiwa kutoelewana. Tazama video hiyo hapa chini;

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents