Habari

China kuifuta sera ya kuzaa mtoto mmoja

Serikali ya China imeamua kuifuta sera yake ya kuzaa mtoto mmoja tu iliyodumu kwa kipindi kirefu.

China

Sera hiyo ilianzishwa mwaka 1979 ili kupunguza ongezeko la watu katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi duniani. Hadi sasa China ina watu zaidi ya bilioni 1.357.

Wapenzi waliokiuka sheria hiyo walikuwa wakiadhibiwa, kupigwa faini, kupoteza kazi na kulazimika kutoa mimba.

Kwa sasa wapenzi wote nchini China wataruhusiwa kuwa na watoto wawili.

Hata hivyo wataalam wamedai kuwa hatua hiyo inaweza kuwa imechelewa tayari kwakuwa imejikuta ikikosa vijana wengi wa kufanya kazi kuendelea kukuza uchumi wake mkubwa. Kuna ongezeko kubwa la wazee.

Serikali bado haijatangaza muda maalum wa sera hiyo kuanza lakini utekelezaji wake utakuwa wa taratibu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents