Burudani ya Michezo Live

China: Wanafunzi kufundishwa kusoma kwa kasi ya ajabu, dakika 5 mtoto kumaliza maneno Laki 1, elimu yahofiwa kushuka

Muingereza Dan Holloway ndiye anayeongoza kusoma haraka zaidi Ulaya. Aliweza kuonyesha uwezo wake wa kusoma maneno 1,700 kwa dakika moja katika mashindano ya mwaka 2018.

Chinese kid flipping the pages of a book

Kituo cha mafunzo ya ziada nchini China, kinajaribu kuwafundisha watoto kusoma haraka kama Holloway: Kituo hicho kinadai kuwa kinaweza kuwafundisha wanafunzi kuwa na uwezo wa kusoma maneno laki moja kwa ndani ya dakika tano.

Lakini mafunzo haya ya kuonyesha mbinu za kusoma kwa kasi yamekuwa na utata, baada ya video inayomunyesha mwanafunzi anavyofungua karatasi za kitabu kwa kasi kusambaa kwa watu wengi huko Beijing.

Utafiti

Katika mashindano haya, wanafunzi wanasoma vitabu kama kadi kwa kuzichanganya.

Namna ya kusoma namna hiyo ni kufungua kurasa kwa haraka na picha ndio inaweza msaidia msomaji kuelewa maudhui ya kile anachokisoma.

Mbinu hiyo ya imekosolewa na wengi na kudaiwa ni ulaghai tu. Mamlaka ya elimu imetoa angalizo kwa kutoa tamko kusema kuwa ni marufuku kwa shule za awali au sekondari kufundisha masomo ya aina hiyo.

Vilevile watafanya utafiti kujua ni kina nani wanaofundisha wanafunzi masomo hayo ya kusoma kwa haraka.

Hofu

Wataalamu wa elimu wanahofia kuwa mafunzo ya namna hiyo yanawapotosha watu, lakini mafunzo hayo tayari yamepata umaarufu kutoka kwa watu wengi tayari kwa sababu tofautitofauti.

Hofu inyoonekana kwa sasa ni kuwa na kiwango kidogo cha masomo ya sayansi na ukosefu wa kutumia kanuni pamoja na mapungufu mengine, ndio maana serikali imewataka wazazi na wanafunzi nchini China kulenga kupata elimu bora.

Mafunzo haya ya kusoma kwa kasi yalianzishwa nchini Japan na mwalimu Yumiko Tobitani, ambaye alichapisha kitabu chake cha mbinu za kusoma mwaka 2006.Chinese school kids in classWataalam wa elimu wamekosoa vikali mafunzo haya na kudai kuwa yatashusha kiwango cha elimu ya sayansi

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya China, kampuni zinazotoa huduma hiyo ya mafunzo ziko kwenye miji mikubwa kama Beijing, Shenzhen, Guangzhou na Hangzhou.

Gharama ya mafunzo hayo huwa ni kati ya fedha za kimarekani dola 4,200 hadi 8,500. Gharama kubwa zaidi ya ada ambayo meja anaweza kulipa sio zaidi ya dola 14,000.

Wachina wengi wamewadhihaki wazazi wanaowapeleka watoto wao kwenye mafunzo hayo.

Bwana Xiong Bingqi, mkurugenzi msaidizi wa taasisi ya utafiti wa elimu katika karne ya 21 ameiambia BBC kuwa mbinu hiyo inakosa mbinu za kisayansi na iko kinyume na utaratibu wa kawaida wa elimu na kutozingatia uelewa wa mwanafunzi.Wallet full of Chinese money billsMteja anaweza kulipia hata dola 14,000

Ujuzi mdogo wa kisayansi

Bwana Chu Zhaohui,mtafiti wa elimu ya sayansi ameiambia BBC kuwa mafunzo hayo yamekosa kutoa ujuzi wa kisayansi, jambo ambalo inabidi walaumiwe.

Anasema kuwa mafunzo hayo yanashindwa kuhusisha wazo la sayansi na uwezo wa kisayansi wa kuhusisha mamboUshindani ni mkali nchini Uchina na wasiwasi wa wazazi juu ya matokeo ya kitaalam unaelezea mahitaji ya mafunzo ya ziadaUshindani mkali nchini China unawapa wazazi hofu juu ya matokeo ya watoto wao ndio maana wanatafuta mafunzo ya ziada

“Watoto wengi huwa wanawadanganya wazazi kuwa taarifa ambazo zimeandikwa kwenye magazeti zinapotosha na masomo hayo yanachangamsha ubongo. Jambo ambalo haliwezekani kabisa,” Chu alisema.

Lakini wazazi watawezaje kuepuka uongo huu wa mbinu za kurahisisha upatikanaji wa ujuzi?

Xiong Bingqi anaamini kuwa kampuni zinazotoa mafunzo hayo zinapaswa kuwa chini ya uangalizi mkubwa, vituo vingi vya mafunzo hayo havijajisajili kwa kuzingatia taratibu za elimu nchini humo.

Aidha bwana Chu anadhani kuwa kubadilisha mfumo wa elimu nchini humo kunaweza kusaidia.'Mfumo wa elimu China ukibadilishwa unaweza kusaidia'Mfumo wa elimu China ukibadilishwa unaweza kusaidia’

Kuna namna moja ya kuleta mabadiliko ya kutathmini uelewa wa masomo.

Bwana Chu amedai kuwa mbinu hiyo ya mafunzo inauwa fursa za wanafunzi katika kujifunza na kuelewa.

“Wazazi na wanafunzi wanakuwa wanazingatia kupata alama za juu badala ya kuzingatia ujuzi”.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW