Habari

China yalipiza kisasi kwa kuongeza ushuru bidhaa za Marekani

China imesema leo kuwa itaongeza ushuru kwa bidhaa za Marekani za thamani ya dola bilioni 60 kuanzia Juni mosi, katika hatua ya kujibu duru ya karibuni ya Marekani kuongeza ushuru kwa bidhaa za China na mipango ya Marekani kuzilenga bidhaa zote zinazoingizwa nchini mwake kutoka China.

Tangazo hilo limekuja baada ya mazungumzo ya karibuni kabisa ya biashara kati ya Marekani na China kumalizika Ijumaa bila makubaliano, na baada ya Marekani kuongeza ushuru kwa bidhaa za China za thamani ya dola bilioni 200.

Licha ya hatua hiyo ya kulipiza kisasi, China imeonekana kutoa muda zaidi wa hadi Juni mosi. Ushuru mpya utazilenga bidhaa kadhaa za Marekani kuanzia asilimia tano hadi 25.

Jibu la China limetangazwa mara tu baada ya Trump kuionya kutolipiza kisasi. Awali, msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya China Geng Shuang alisema kuwa China hitawahi kusalimu amri kwa shinikizo la kimataifa.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents