DStv Inogilee!

China yasitisha matumizi ya ndege za Boeing 737 MAX 8, ni baada ya ajali ya Ethiopian Airlines

China imeagiza kampuni zote za ndege nchini humo kusitisha safari za ndege aina ya Boeing 737 Max 8 baada ya ajali ya ndege ya Ethiopia ambayo ni ya muundo sawa na hizo.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la BBC, Kampuni za ndege ni lazima zisitishe usafiri wa abiria wa ndege zote za Boeing 737 Max 8 kufikia saa 18:00 kwa saa za huko. Ilisema taarifa kutoka halmashauri ya usafiri wa ndege ya China.

Ajali ya Ethiopian Airlines ni ya pili ya ndege aina hiyo chapa 737 Max 8 katika muda wa miezi mitano iliyopita.Boeing 737 Max-8 ni ndege ya aina gani?

Ethiopian Airlines: Uraia wa abiria waliokufa watambuliwa

Taarifa kutoka halmashauri ya usafiri wa ndege China, imesema, huduma za ndege hiyo zitarejelewa baada ya ”kuthibitisha hatua za kiusalama zimeimarishwa”

Mamlaka hiyo pia imesema itashauriana na halmashauri ya safari za ndege nchini Marekani na wasimamizi wa Boeing.

Taarifa hiyo pia ilisema kuwa raia wanane wa China walikuwa wameabiri ndege iliyohusika katika ajali ya siku ya Jumapili ikiwa safarini kutoka Ethiopian kuenda Kenya iliyoanguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka mjini Addis baba.

Eneo la tukio

Pia ilitaja ndege ya Indonesia ya Lion iliyoanguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka mjini Jakarta mwezi Oktoba na kuwaua abiria wote 189.

China ni soko kubwa la kampuni ya kunda ndege ya Marekani na ni moja ya mataifa iliyo na ndege nyingi aina ya Boeing 737 MAX-8.

Kampuni hiyo imeiuzia shirika la ndege la China ndege 76 aina ya Boeing 737 MAX, na tayari ilikuwa imeagiza ndege zingine 104, kwa mujibu wa data kutoka mtandao wa kampuni ya Boeing.

Boeing kwa ushiriakiano na shirika la ndege la kibinafsi la China (COMAC) inaendesha kituo cha kutengeza muundo wa ndani wa ndege za 737 MAX katika mji wa mashariki wa Zhoushan.

Kampuni hiyo imewasilisha ndege za kwanza za MAX 8 kwa shirika la ndege la China mwezi Decemba.

Ndege hizo zina zinaunganishwa Renton, jimbo la Washington, na kisha kupelekwa Zhoushan kukamilisha muundo wa ndani kwa mujibu wa Boeing.

Shirika la ndege la Ethiopia limetangza kusitisha safari za ndege zake zote chapa Boeing 737 Max 8 kuanzia jana Machi 10 hadi taarifa zaidi itakapotolewa.

Shirika hilo lisema kwamba licha ya kuwa chanzo cha ajali hakijajulikana, wameamua kuchukua hatua hiyo kama tahadhari ya ziada.

Mambo 7 makuu kuhusu Boeing 737 Max-8

  • Boeing 737 Max-8 imekuwa katika safari za kibiashara tangu mwaka 2017.
  • Injini yake iko mbele kidogo na juu kiasi na usawa wa mbawa zake, ikilinganishwa na muundo wa awali wa ndege za Boeing.
  • Kifaa cha kubaini ajali na kazi ya programu inayoendesha kazi hiyo inafanya kazi tofauti na ile ya miundo ya awali ya Boeing 737.
  • Ndege iliyoanguka ni miongoni mwa sita kati ya 30 zilizoagizwa na shirika la ndege la Ethiopia kwa upanuzi wa shirika hilo.
  • Ajali nyingine ya ndege kama hiyo ya shirika la Lion Air ambayo pia ilikuwa mpya ilitokea muda mfupi baada ya kuondoka.
  • Boeing ilisema imetuma ilani ya dharura kwa kampuni za ndege ikionya kuhusu matatizo ya mfumo wa kuzuia ndege kukosa nguvu.
  • Katika ajali ya nyuma, marubani walionekana kutatizika na mfumo huo wa kujitegemea ulioundwa kuizuia ndege hiyo kukwama, ulioidhinishwa katika Boeing 737 Max.


Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW