Habari

China yathibitisha kuzuia mkuu wa Polisi wa kimataifa (Interpol) aliyepotea

China yathibitisha kuzuia mkuu wa Polisi wa kimataifa (Interpol) aliyepotea

Beijing imesema alikuwa anachunguzwa na tume ya kupambana na rushwa nchini humo kwa ukiukaji wa sheria. Meng, ambaye pia ni naibu waziri wa wizara ya usalama wa umma China, aliarifiwa kupoeta baada ya kusafiri kutoka mji wa Lyon Ufaransa , kuliko na makao makuu ya Interpol kwenda China mnamo Septemba 25.

Interpol imesema imepokea barua ya kujiuzulu kwake mara moja kutoka kwa ofisi ya rais. Familia yake Meng haijawasiliana naye tangu andoke katika makao hayo makuu ya Interpol nchini Ufaransa Gazeti la South China Morning Post lilikunuu taarifa zilizosema kuwa Bw Meng, 64, alipelekwa kwenda kuhojiwa nchini China.

Haijulikani ni kwani nini alikuwa anachunguzwa na mamlaka za nidhamu au alikuwa anazuiliwa wapi. Mapema wiki hii mwanafilamu Fan Bingbin, ambaye alitoweka nchini China, aliibuka akiomba msamaha na faini ya dola milioni 129 kwa kukwepa kulipa kodi na makosa mengine.

Alichaguliwa rais wa Interpol mwezi Novemba mwaka 2016, raia wa kwanza wa China kuchukua wadhifa huo na anatarajiwa kuwa katika wadhifa huo hadi mwaka 2020. Yeye ni mkuu wa kamati kuu cha shirika hilo ambalo hutoa mwongozo mzima wa Interpol.

Kabla ya kuchukua wadhifa huo, Bw Meng alikuwa naibu waziri wa masuala ya usalama wa umma nchini China na bado yeye ni mwanachama wa cheo cha juu wa chama cha Communist.

Pia ana ujuzi wa miaka 40 ya ujuzi wa sheria ya uhalifiu nchini China hasa katika nyanja za madawa ya kulevya, ugaidi na udhibiti wa mipaka. Baada ya kuchaguliwa kwake makundi ya haki za binadamu yalielezea wasi wasi kuwa hatua hiyo itaisadia China kuwatafuta watoro wa siasa ambao waliikimbia nchi.

Chanzo BBC

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents