Habari
Chingy ndani ya Leaders!
Inasemekana kwamba msanii wa Hip Hop kutoka Marekani Chingy atadondoka Bongo wiki ijayo na kutumbuiza katika onesho ndani ya Leaders Club.
Gumzo ni kwamba onesho hilo litafanyika Jumapili tarehe 5 April 2009 ndani ya viwanja vya Leaders Club, tutawaletea habari zaidi punde tukipata. Kwa sasa upelelezi unaendelea! Anayejua zaidi juu ya hilo anakaribishwa kuchangia.