Burudani

Chipukeeyz wa Kenya awatamanisha Idris na Mc Pilipili

By  | 

Mchekeshaji na kutoka Kenya Chipukeeyz amewatamanisha wachekeshaji wengine wa Afrika Mashariki.

Chipukeezy ambaye yupo Marekani kwa sasa amekutana na mchekeshaji maarufu duniani Kevin Hart maeneo ya Hollywood na kupata nafasi ya kupiga naye picha huku akiwa ameshika kitabu cha ‘I Can Make This Up’ cha Hart ambacho amekizindua siku chache zilizopita.

Kupitia mtandao wa Instagram, Chipukeey ameweka picha hiyo na kuandika, “If you can see it in your mind you will hold it in your hand. This man inspires me and I have always wanted to meet up with him and tell him to his face @kevinhart4real it was a pleasure man. He told me that he can’t wait to see me at the Top #i can’t make this up I can’t wait too Hollywood am coming ???? #comedicidol #comedytings #comedichustle #Godisgood #icantmakethisup.”

Hata hivyo mchekeshaji Idris Sultan aliyekuwa na ndoto ya kufika Hollywood amempongeza Chipu kupitia mtandao huo kwa kuandika “Ila Chipooo you scared Kev ? cheki sura yake. Brothers in art ?? cc: @chipukeezy & @kevinhart4real.”

Naye Mc Pilipili amempongeza kwa kuweka picha ya Hart kwenye mtandao huo na kuandika, “I can’t make up in this life A book from @kevinhart #goals #malengo #mtotowanuru.”

Na Laila Sued

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments