Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Chodry kuachia filamu yake ‘Return to Zero’ akiwa na Hemedy PHD

Baada ya muda mrefu kuonekana movie za Bongo kutofanya vizuri, tuzo walizozipata Lulu na Richie zimeanza kuonesha mwanga kwenye industry ya Bongo Movie.

IMG-20160317-WA0020

Ni bahati sana kwa msanii anayechipukia kupewa nafasi ya kufanya movie na wasanii wakubwa. Diana Nsumba aka Chodry ni miongoni wa wasanii hao waliopata bahati kwa kipindi hicho kwa kufanya movie ya, ‘Julieth’, ‘Only You’ na ‘The Same Script’.

Akiongea na Bongo5, Chodry alisema Baada ya kufanya movie za watu sasa ‘nitaachia movie yangu mpya mwezi huu mwishoni.’

“Nashukuru kwa wasanii walioniamini mwanzo wakanipa nafasi kwenye movie zao nikafanya, baada ya kupata nafasi hiyo nimejifunza mengi na mwezi huu mwishoni nitaachia movie yangu mpya ya ‘Return To Zero’ ambayo ndani yake yupo Hemedy Phd na wasanii wengi wenye uwezo mkubwa,” ameongeza.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW