Burudani

Chris Brown aamua kuondoa nyimbo alizomshirikisha Ex wake Rihanna katika album yake mpya ‘X’

Album mpya ya star wa R&B Chris Brown iko njiani inategemewa kutoka mwezi ujao (July 16) lakini kuna uwezekano usikutane na wimbo wowote wenye sauti ya ex girlfriend wake Rihanna katika album hiyo, kutokana na maamuzi ya Brown ambaye hataki wimbo wowote aliofanya na aliyekuwa babymama wake uwemo katika album hiyo.

chris-brown-studio2

Chanzo kimoja cha karibu kimeuambia mtandao wa Hollywoodlife kuwa kimeona track list ya album hiyo inayoitwa ‘X’ na hakuna wimbo hata mmoja alioshirikiana na Rihanna uliowekwa japo zipo nyimbo kadhaa walizorekodi pamoja na kali.

Ameongeza kuwa ma executives wanaohusika na album hiyo wamemshauri Chris asiiondoe duet yake na Riri, lakini mkali huyo amesisitiza kuwa hataruhusu hata wimbo mmoja aliofanya na Riri uingie katika album ya ‘X’, na akaongeza ataikagua album kabla ya kuiruhusu kutoka.

Wahusika hao bado wanaamini kuwa huenda Chris atabadili mawazo au ikishindikana watamuongeza malipo ili abadili mawazo sababu wanahisi kuwa ushirikiano wake na Riri unaweza kuwa hit.

Chris mwenye miaka 25, (March) mwaka huu alipozungumza na USA Today aliahidi kuwa wimbo aliofanya na Rihanna utakuwepo katika album yake mpya ya ‘X’, lakini hiyo ilikuwa ni ahadi ya kabla mapenzi yao hayajavunjika. “We’re taking it one day at a time. She’s a wonderful girl. She’s beautiful. She’s on tour and our schedules don’t allow us to be as close as we want to be. But everything is good. She will be on my album,”.Alisema Breezy, lakini yote hayo yameyeyuka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents