Burudani

Chris Brown afungua kesi kupigania kumchukua mwanae Royalty

Chris Brown anamtaka mwanae Royalty. Muimbaji huyo amewasilisha nyaraka za kisheria mjini Houston kutaka kuwa baba halali wa mwanae huyo mwenye umri wa mwaka mmoja.

chris-royalty-bbma

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, Breezy na mama wa mtoto huyo, Nia Guzman wamekuwa wakipishana kuhusiana na mahitaji ya mtoto huyo hivyo anamtaka jaji amtambue kama baba halali wa mtoto huyo, hatua ambayo itampa haki ya kupambana na Nia juu ya mtoto huyo.

Chris anadaiwa kumlipa Nia kile anachoamini ni kiasi sahihi kwa mwezi ambacho ni dola 2,500 kwa mwezi japo anataka apewe $15,000 kwa mwezi ili kumtunza mtoto.

Muimbaji huyo pia anataka apewe uhuru wa kumuona mwanae kwakuwa Nia anadaiwa kumnyima haki ya kumuona.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents