Burudani

Chris Brown aigomea serikali kufuta Graffiti aliyoichora nje ya nyumba yake kwa madai kuwa inalindwa na katiba ya Marekani!

Siku chache zilizopita majirani wanaoishi karibu na makazi ya mwimbaji wa R&B Chris Brown walilamika kuhusiana na Graffiti iliyochorwa na msanii huyo kwenye ukuta wa uzio wa nyumba yake wakidai inawatisha watoto wao ambao hupita eneo hilo.

Neighbors complain! Chris Brown paints graffiti on his house

Baada ya watu hao kupeleka malalamiko yao kwenye vyombo vya sheria, jiji la Los Angeles lilimshitaki Breezy kwa kuchora Graffiti hiyo bila kupewa kibali.

Kwa mujibu wa TMZ ambao wamefanikiwa kuziona nyaraka za kesi hiyo, Brown amekata rufaa na kuwaambia kuwa serikali haina haki ya kumlazimisha kufuta graffiti hiyo katika ukuta wa nyumba yake iliyoko Los Angeles kwasababu inalindwa na katiba ya Marekani.

“The murals are a reflection of [my] aesthetic taste and a reflection of free speech and expression protected by the First Amendment to the United States Constitution.”

Kesi hiyo hivi sasa iko chini ya ‘Dept. of Building and Safety’s board of appeals’ na endapo atashindwa anaweza kwenda katika mahakama ya juu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents