Burudani

Chris Brown aitwa mahakamani

Chris Brown amepewa amri ya kwenda mahakamani mwezi ujao kama sehemu ya utaratibu aliowekewa kuangaliwa maendeleo ya kifungo chake cha nje kilichotokana na kumpiga mpenzi wake wa zamani, Rihanna.
Ingawa jana hakwenda mahakamani hapo, jaji Patricia Schnegg, ameonesha wasiwasi wa uhalali wa masaa aliyoyatumia mshindi huyo wa tuzo za Grammy kufanya kazi za jamii na wapi anakozifanyia.
Jaji huyo ameiagiza idara ya probation kutafuta ni wapi Chris anaishi kwakuwa anamiliki nyumba jijini Los Angeles, California na amekuwa akifanya kazi hizo kwenye jimbo alilotokea la Virginia.
Pia jaji huyo anataka ufanyike ukaguzi wa masaa aliyofanya kazi hizo na kumtaka aende mahakamani hapo August 21.
Brown ameruhusiwa kufanya kazi hizo kwa miezi sita jimboni kwake Virginia, lakini jaji amewataka maafisa wa probation jijini Los Angeles kupitia rekodi ili kutambua ni kazi gani aliyofanya.
Kazi anazotakiwa kufanya Chris Brown ni pamoja na kusafisha kuta zilizochorwa graffiti,kufagia barabara na kazi zingine za mikono.
Brown, 23, bado yupo kwenye probation kutokana na tukio hilo la kumpiga Rihanna February 2009 na tayari amemaliza kupewa ushauri kuhusu ukatili wa nyumbani na namna ya kuzuia hasira.
Hata hivyo hakukutajwa ugomvi wake wa hivi karibuni na Drake uliotokea mwezi uliopita kwenye klabu ya usiku ya jijini New York.
Mwanamuziki huyo anatumikia kifungo cha nje cha miaka mitano.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents