Burudani

Chris Brown asikitika baada ya Rihanna kushambuliwa kwa chupa na shabiki jijini London

riri mguu

Chris Brown alifarijika baada ya kusikia kuwa mpenzi wake Rihanna ni mzima wa afyya baada ya mtu mmoja kumponda na chupa ya kinywaji cha Lucozade na kumfanya aanguke chini.

Mtu huyu aliponda chupa hiyo ambayo hata hivyo haikumpata Rihanna huku akilitaja jina la Chris wakati Rihanna alipokuwa akitoka kwenye klabu ya usiku ya The Box ya jijini London, Uingereza akiwa na rafiki yake Cara Delevingne juzi Jumamosi.

Chanzo kimoja kimeuambia mtandao wa HollywoodLife.com kuwa Chris anampenda sana Rihanna na hawezi kukubali mtu amchezee ama kumuumiza kwa aina yoyote ile.

Chris na Rihanna walipokuwa pamoja kwenye tuzo za Grammy
Chris na Rihanna walipokuwa pamoja kwenye tuzo za Grammy

Tukio hilo lilimsababishia Rihanna apate mchubuko kwenye goti lake na pia mlinzi wake kuumia mguu alipokuwa akijaribu kumkamata mtu huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents