Burudani

Chris Brown atingia list moja na Rihanna

By  | 

Msanii asiyeishiwa vituko mbali mbali Chris Brown, hatimaye amekaribishwa rasmi na mtandao wa Youtube katika list ya wasanii waliotunukiwa Diamond Play Button.

Mtandao huo wa Youtube umemzawadia Chris ‘Diamond Play Button’ baada ya kufikisha watazamaji milioni 10. Chris aliamua kushare ujumbe na zawadi hiyo kutokea Youtube kupitia Instagram yake.

Kwa maana hiyo Chris anaingia list moja ana aliyekuwa mpenzi wake Rihanna, Taylor Swift, Skrillex, Ariana Grande na kwa upande wa Hip hop Nicki Minaj, Wiz Khalifa, na Eminem. Hawa wote waliwahi kuzawadiwa na Youtube kwa kuvuka watazamaji milioni 10.

Na Laila Sued

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments