Burudani

Chris Brown atupwa jela, ni baada ya kuzingua rehab

Chris Brown ametupwa jela baada ya kukiuka agizo la jaji la kuendelea kukaa rehab. Ijumaa asubuhi, muimbaji huyo mwenye miaka 24 alifukuzwa kwenye rehab hiyo iliyopo Malibu nchini Marekani ambako amekaa kwa karibu miezi minne.

Chris+Brown+Chris+Brown+Arrives+Court+Hearing+_1-lX99MgrXl
Jaji anayesimamia kesi yake ya kumpiga Rihanna, alimuagiza Brown kuendelea kukaa rehab kwa siku 90 ili kusaidiwa kupunguza hasira ambako alimaliza mapema mwezi huu. Hata hivyo, mwishoni mwa mwezi uliopita jaji huyo aliamuru msanii huyo aendelee kukaa rehab kwa miezi miwili mingine.

Haijulikani kwanini amefukuzwa rehab lakini mtandao wa TMZ umedai kuwa amekiuka baadhi ya sheria za ndani japokuwa hazihusiani na madawa ya kulevya ama fujo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents