Burudani

Chris Brown kuwahamishia mwanae na mama yake nyumbani kwake L.A

Chris Brown amepanga kumchukua mwanae pamoja na mama yake na kuishi nao nyumbani kwake, mtandao wa Hollywood Life umesema.

royalty-baby-pic
Mtoto wa Chris Brown, Royalty

Chris Brown, 25, anataka mwanae wa kike mwenye umri wa miezi tisa, Royalty na mama yake, Nia Amey, 31 kuhama kutoka Houston wanakoishi sasa, ili waishi naye nyumbani kwake jijini Los Angeles.

royalty-chris-brown-daughter-gallery-1

Kwa mujibu wa vyanzo vilivyoongea na mtandao huo, Chris anataka kusherehekea siku yake ya kuzaliwa kutimiza miaka 26 akiwa na Royalty.

Chris anataka kuhakikisha kuwa anamuona mwanae kila siku.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents