Burudani

Chris Brown na Rihanna: Jay-Z hana tatizo nao tena


Inaonekana kama vile Jay-Z ameamua tu kuwa mpole kutokana na urafiki usioisha wa Rihanna na Chris Brown.
Mfanyabiashara mwenzie na Jay-Z wa Roc Nation, Jay Brown amesafiri hadi nchini Barbados kumjulia hali mwanamuziki huyo baada ya kumaliza likizo yake ya barani Ulaya.
Bosi huyo wa record label ya Roc Nation ameamua kumtembelea Rihanna kufuatia ripoti kuwa wapenzi hao wa zamani wameanza kuwa karibi zaidi baada ya Chris kumtembelea Rihanna nchini Ufaransa.
Mrembo huyo alikutana na Chris na kula raha pamoja kwenye meli aliyokodi kwa paundi 100,000 kwa wiki nchini Ufaransa.
Chanzo kimoja kimeliambia gazeti la The Sun: “Jay-Z sees Rihanna like a daughter and has sent his right-hand man Jay to Barbados to see what’s going on with her and Chris.
“Alikubali (Rihanna) kuwa wamerejesha urafiki wao, na Jay alimwambia kuwa wote wapo nyuma yake na wanataka awe na furaha.”

“Chris pia anatarajia kwenda visiwani humo hivi karibuni kumwona. Anajua (Rihanna) kuwa mashabiki wake wengi hawatafurahia kuwaona pamoja – people still haven’t forgiven him.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents