Tupo Nawe

Chris Smalling atoa neno baada ya kumuumiza Messi “Anajua ilikuwa ni ajali kazini”

Beki wa Manchester United Chris Smalling amefunguka mengi baada ya mchezo wao wa klabu bingwa barani Ulaya UEFA ambapo lilitokea tukio la kumuumiza winga wa klabu ya FC Barcelona na raia wa Argentina Lionel Messi katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Old Trafford ambapo United walipoteza kwa kufungwa goli 1-0 nyumbani.

Baada ya tukio hilo Smalling aliongelea na kusema kuwa:- “Tulizungumza baada ya mchezo na tulikuwa na majadiliano mafupi na tukapeana mikono.

“Anajua ilikuwa ni ajali tu.”

Alifafanua zaidi juu ya changamoto ya angani ambayo imesalia mpinzani wa Argentina, Smalling alisema: “Sikujua wakati ambao niliruka kuwania mpira kama ningemgusa”

“[Luis] Suarez [alikuja kwangu] baada ya mchezo pia. Tulikuwa na tussle nzuri na alinipa mkono baadaye na kusema ‘Kila la kheri’.

“Kwa upande wangu ni nzuri sana wakati unaweza kuwa na vita hiyo kwenye kwenye na kisha baada ya mchezo kunakuwa na heshima sababu, kila mtu anataka na anajitahidi kufanya vilivyo bora zaidi katika upande wake.”

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW