Michezo

Chris Wood avunja rekodi Burnley

Aliyekuwa mchezaji wa klabu ya Leeds United, Chris Wood amefanikiwa kuvunja rekodi ya usajili ya Burnley baada ya kusaini mkataba wadau la paundi milioni 15 ambayo itamfanya kuwepo hapo kwa miaka minne.

Wood mwenye umri wa miaka 25 amevunja rekodi iliyowekwa hapo awali ya paundi milioni 13 iliyowekwa na mchezaji Robbie Brady aliyesajiliwa mwezi Januari.

Mchezaji huyo raia wa New Zealand alifanikiwa kufunga mabao 44 kati ya mechi 88 alizoichezea Leeds akitokea Leicester City ya nchini Uingereza mwezi Julai 2015

Raia huyo waNew Zealand alijiondoa kutoka kwa mechi ya Leeds dhidi ya Sunderland katika ligi ya daraja la pili Jumamosi uvumi kuhusu kuhama kwake ulipokuwa umesheheni.

Wood anaruhusiwa kuchezea Burnley katika Kombe la EFL kwani alikuwa benchi na hakuchezeshwa mechi waliyoilaza Port Vale.

Wood,ambaye anakuwa mchezaji wa sita kununuliwa na Meneja, Sean Dyche katika kipindi hiki cha usajili.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents