Burudani

Christian Bella aanza kuwika Congo (Video)

Mkali wa masauti, Christian Bella ambaye ni raia wa Congo, ameanza kufanya vizuri zaidi nyumbani kwao, Congo baada ya kufanya vizuri nchini Tanzania.

Muimbaji huyo wiki hii alitembelea nchini humo kwaajili ya show na kupokewa kwa shangwe kubwa.

“Nabii anae kubalika kwao (Congo Uvira,” aliandika Instagram Christian Bella akiambatanisha na video.

https://www.instagram.com/p/BUYlpaMBQRq/?taken-by=bellachristian1

Muimbaji huyo mwaka 2016 aliweza kufanya kolabo na msanii mkongwe wa Congo, Koffi Olomide, lakini kolabo hiyo haikuweza kufanya vizuri nchini humo.

Mapema mwaka jana muimbaji huyo alisema kuwa muziki wa Congo ni mgumu kupata nafasi kutokana nakuwa na wanamuziki wengi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents