Shinda na SIM Account

Christian Bella ajipa tano na Alikiba, adai wanatoa ngoma bila kiki

Msanii wa muziki Bongo, Christian Bella amesema yeye na Alikiba ni miongoni mwa wasanii wasiyokuwa na kelele nyingi pindi wanapoachia ngoma zao.

Muimbaji huyo amesema wasanii waliotoka kuanzia mwaka 2006 hadi 2010 wengi wanakuwa na utaratibu huo huku akijitolea mfano yeye na Alikiba.

“Sisi hatunaga zile kelele kuwa umeachia wimbo mpya, naachia wimbo watu taratibu unakuwa wenyewe lakini nikitoa wimbo unapendwa nina fan base kubwa, wapenda muziki wapo wengi sana” amesema Bella.

“Wanaopenda muziki bila kiki wapo wengi sana, siyo mpaka ufanye tukio ndio watu wakupe tension kuna watu ambao wanaheshimu huu muziki, sisi tunatumia vipaji bila tension, tunatumia real talent” Bella ameiambia Bongo5.

Christian Bella anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Shuga Shuga’ ambayo imetoka leo.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW